Burudani ya Michezo Live

Ratiba ya UEFA yapangwa, Man City, Real Madrid Juventuvs vita mpya huku Chelsea, Bayern na Barcelona

Klabu ya Manchester City ya England ambayo inaongoza kwa bao 2-1 dhidi ya Real Madrid,itamvaa mshindi kati ya Lyon na Juventus ya Italia ambapo katika mchezo wa kwanza wafaransa waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Droo ya ligi ya mabingwa Ulaya ikiwekwa hadharani hii leo.

Manchester City inahitaji sare ya aina yoyote ili ifuzu hatua ya robo fainali,matokeo ambayo hata Lyon inayahitaji katika mechi ya marudiano itakapokua ugenini nchini Italia

Nayo Barcelona ambayo katika mechi ya mkondo wa kwanza ililazimisha sare ya bao 1-1 na Napoli huko nchini Italia,nayo itahitaji suluhu au ushindi kwenye mchezo wa marudiano na iwapo itafuzu itacheza na mshindi kati ya Bayern Munich na Chelsea.

Ikumbukwe Bayern ilishinda bao 3-0 dhidi ya Chelsea katika mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa jijini London,hivyo inahitaji ushindi,sare au kupoteza kwa mabao chini ya matatu itafuzu hatua ya robo fainali.

Katika droo iliyipangwa leo,Atalanta ya Italia itakipiga dhidi ya Pari St Germain ya Ufaransa huku RB Leipzig ya Ujerumani ikikabiliana na Atletico Madrid ya Hispania.

Kwa mujibu wa shirikisho la soka Ulaya UEFA ni kwamba mechi za marudiano za 16 bora ambazo hazikuchezwa kutokana na janga la Corona sasa, sasa zitapigwa August 7 na 8 bila ya mashabiki.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW