Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Ray C: Kiuno bila mfupa kinaanza kurejea (Picha)

Miaka takriban mitano iliyopita, Rehema Chalamila aka Ray C alikuwa akijulikana kwa kiuno chake bila mfupa na alikuwa mrembo haswaa.

10985977_724329164349102_164392917_n

Lakini mambo yalibadilika baada ya kurejea tena kutoka kwenye tatizo la uraibu wa madawa ya kulevya na kuanza kutumia dawa ziitwazo Methadone ambazo zilimfanya anenepe kwa kiasi kikubwa kiasi cha kumfanya asiwe na kiuno chenye mfupa tena.

10979555_889208161131153_174652242_n

Hata hivyo muimbaji huyo amedhamiria kurudi tena kwenye muonekano wake wa zamani kwa kufanya mazoezi makali na kutumia lishe maalum.

11008104_433757660115668_110641588_n

“20kg to go!Safari ya kupunguza mwili bado inaendelea, nashukuru nimeanza kuona mwanga mbele yangu,” ameandika Ray C kwenye picha aliyoweka Instagram inayoonesha kuwa jitihada zake zimeanza kuzaa matunda.

10985995_1553162421635300_1101089611_n

“Si rahisi ila nimezoea kupambana na lolote mbele yangu na na uhakika ntashinda na hili pia. Am doing ths for all my fans around the world,” ameongeza.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW