Habari

RC Anna Mghwira atii agizo la Makamu wa Rais

By  | 

Mkuu wa Mkowa wa Kilimanjaro, RC Anna Mghwira ametii agizo la Makamu wa Rais, Bi Samia Suluhu Hassan la kuwataka wananchi kujitokeza kufanya mazoezi nchini.

RC Mghwira ametoa agizo hilo ofisini kwake mjini Moshi, ambapo amesema kuwa mazoezi hayo yatafanya wananchi wafahamiane lakini pia kwaajili ya afya zao.

“Naomba tufanye mazoezi kila Jumapili ya pili ya mwezi na naomba na sisi tutekeleze agizo hili kwa kufanya mazoezi kwa muda wa saa moja kuanzia saa 12 mpaka saa 1 tunafanya mazoezi ili tufahamiane lakini pia kwaajili ya afya zetu lakini pia ni kupambana na magonjwa ambayo hayaambukizi kwahiyo napenda kuwatangazia wakati wote wa mkoa wa Kilimanjaro wale walioko Moashi mjini tutakutania ofisi ya Mkuu wa mkoa tuaanzia hapo na kwenda maeneo ambayo tutakuwa tumepangiwa kwa waliopo wilayani katika wilaya zetu 6 tutakutana ofisi za wakuu wa wilaya na mazoezi yataanzia hapo na routes zitapangiwa kwa kila wilaya,” alisema RC Mghwira.

“Naomba sisi sote tushiriki zoezi hili mazoezi haya yawe sehemu ya kuimarisha umoja wetu undugu, umoja na ushirikiano tulio nao kama mkoa naomba watu wote tuchangamkie jambo hili litupe furaha litupe amani, litupe faraja ili kwa pamoja tuweze kushiriki azma hii”.

Disemba Mwaka jana, Bi Samia alitoa agizo kuwa kila Jumamosi ya pili ya mwezi iwe siku ya mazoezi nchini.

Na Emmy Mwaipopo

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments