Habari

RC Makonda akabidhi magari 18 kwa Jeshi la Polisi Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda Jumapili hii amekabidhi magari ya kisasa 18 kwa  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa. Magari hayo ni kati yale 26 yaliyopelekwa Mkoani Kilimanjaro yakiwa mabovu kwaajili ya kufufuliwa upya.

RC Makonda akiwa na Kamanda Mambosasa Mkoani Kilimanjaro

Magari hayo  yamerudishwa Dar es salaam yakiwa mazima  huku yakionekana kama magari ya UN ambapo yatakuwa na uwezo wa kubeba askari 11 wakiwa wamekaa na silaha zao.

Akikabidhi magari hayo kwa Jeshi la Polisi, RC Makonda amesema yataenda kuhudumia wananchi kwa kuimarisha Ulinzi na Usalama jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa kilichomgusa kuboresha Jeshi la Polisi ni baada ya kuona askari wakifanya kazi katika mazingira magumu na wakati mwingine kuvamiwa na majambazi kisha kuuawa na kuporwa Silaha.

RC Makonda akiendesha moja kati ya magari hayo

Aidha RC Makonda ameishukuru kampuni ya Rajinder Motors Ltd (RSA) kwa kumuahidi kutengeneza Magari 56 ya Polisi Dar es Salaam bila kutumia fedha za serikali (Bure).

Makonda ametumia makabidhiano hayo kutuma salamu kwa Majambazi, vibaka na wale wenye nia ya kuvuruga Amani na Usalama kuwa kiama chao kimefika.

Amesema alipotangaza mpango wa kufufua Magari yaliyokufa wapo waliombeza lakini sasa wanajionea Magari yakiwa Mapya.

Makabidhiano hayo yameshuhudiwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mgwira, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar ea Salaam, Lazaro Mambosasa na viongozi wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama ambapo wamempongeza RC Makonda kwa ubunifu mkubwa alionao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents