Habari

RC Makonda: Bodaboda na bajaj ziingie mjini kipindi hiki cha Corona (Video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo April Mosi ameruhusu Pikipiki na Bajaji kuingia katikati ya Jiji kwaajili ya Kubeba Abiria kwa Sharti la kuhakikisha wanavaa Kofia ngumu (helmet) na kutokuingia katika Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi hadi Ugonjwa wa Corona utakapomalizika.

https://www.instagram.com/p/B-cK0faBwu1/

RC Makonda amefikia uamuzi huo baada ya kushuhudia adha ya Usafiri wanayopata Wananchi kufuatia agizo la Daladala zote kutakiwa kutozidisha abiria (level seat) jambo lililosababisha baadhi ya abiria kuchelewa kazini, kuachwa kwenye vituo na tatizo la msongamano wa watu vituo vya daladala.

Aidha RC Makonda ameielekeza Mamlaka ya Usimamizi wa usafiri wa Ardhini (LATRA) kuhakikisha inakutana na Chama cha Wamiliki wa Daladala ili wafanye mabadiliko ya Route za Daladala kabla ya kesho saa sita mchana baada ya kubaini kuwepo kwa baadhi ya Wamiliki wa Daladala walioamua kusitisha kutoa huduma za usafiri kutokana agizo la serikali kutaka Daladala zisijaze abiria.

Pamoja na hayo RC Makonda amewaomba wamiliki wa Nyumba, Apartments, Fremu za biashara na Ofisi kupunguza kodi kwa 50% kwa kipindi hiki ambacho uchumi wa watu umeyumba kutokana na janga la Corona ambapo hadi sasa zaidi ya Wamiliki 50 wa nyumba wamekubali kupunguza kodi.

Hata hivyo RC Makonda amewaomba wananchi kuendelea kuchukuwa tahadhari dhidi ya Corona kwa kuhakikisha wanazingatia maelekezo yote yanayotolewa na Wizara ya Afya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents