HabariUncategorized

RC Makonda kuwainua mabaharia

Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameahidi kutatua changamoto zinazowakabili mabaharia kwa lengo la kuwawezesha mabaharia kupata kazi ndani na nje ya nchi.

RC Makonda akikabidhiwa zawadi na mabaharia

Makonda ameyasema hayo Jumanne hii katika ufunguzi wa mkutano wa mabaharia wa mafunzo ya kuwajengea uwezo uliofanyika katika Ukumbi wa Kajimjee Hall  jijini Dar es salaam.

RC amesema changamoto ambazo zinawakabili mabaharia hao zikitatuliwa zitaweza kutatengeneza fursa za watanzania wengi kuajiriwa na kupewa usalama wa mwajiriwa.

“Naamini changamoto zote hizi ambazo nimeziona zipo kwenye makundi matatu ninaweza kuzitatua na tutaendelea kushirikiana na kuweka mikakati itayowawezesha mabaharia kunufaika, na niwahakikishie kwamba tutafanikiwa.” amesema RC Makonda.

RC Makonda alisema changamoto za kisera za mabaharia hao atazifikisha kwa Rais Magufuli ili zipatiwe ufumbuzi.

Alisema kuna baadhi ya kazi ambazo wanastahili kupewa mabahari wa ndani lakini wananyimwa kutokana na kukosa sera ambazo zitakuwa zinawasimamia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents