Michezo
Real Madrid yachukua ubingwa wa UEFA Super Cup
Real Madrid jana ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya FC Seville kwenye mchezo wa UEFA Super Cup uliopigwa mjini Cardiff kwenye dimba la Millenium.
Real Madrid wakifurahia na taji lao la Super Cup ya UEFA
Kikosi kipya cha Real Madrid kilichotwaa Super Cup
Cristiano Ronaldo alifunga mabao yote mawili na kuipa Real ubingwa huo kwa mara nyingine tangu mwaka 2002. Mchezo huo ulihudhuriwa na mashabiki wapatao 33,500 na alikuwepo pia kocha wa zamani wa Man United, Sir Alex Ferguson.