Soka saa 24!

Rich Mavoko ahoji ‘wanaodhani labda nilikuwa nataka kufa, wapi niliaga kuwa nakufa?’

Msanii wa muziki Rich Mavoko ambaye hivi karibuni aliwashtua mashabiki wake katika mitandao baada ya kujitabiria kifo, ameeleza sababu ya kufanya hivyo.

Katika ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, Mavoko aliandika maneno mafupi yaliyoambatana na picha ikimuonyesha amejiinamia: ‘Ni siku ya mwisho ya maisha yangu yaliyobaki’.

Maneno yaliyoibua gumzo huku wengine wakimtakia apumzike kwa amani kwa kuandika maneno mafupi ya kingereza RIP.

Mavoko ameuambia mtandao wa Mwananchi Digital “Mfano leo ni siku ya Alhamisi (jana), ni wazi kwamba hakuna Alhamisi nyingine kama hii itakayojirudia ndicho nilichokuwa ninamaanisha wakati naandika ujumbe huo na mbona ni vitu vinaimbwa kwenye nyimbo mbalimbali, vinaandikwa kwenye vitabu labda kwa kuwa wengi wetu sio wapenzi wa kusoma.

“Lakini kwa wengine wanaojua kuchanganua mambo nina imani waliposoma neno kwa neno walinielewa nini nilimaanisha na hao wanaodhani labda nilikuwa nataka kufa, wapi niliaga kuwa nakufa?”alihoji Mavoko.

Alipoulizwa kama ujumbe huo hakuleta athari kwa ndugu na watu wake wa karibu, amesema hakupata usumbufu wowote kwa kuwa wanaomjua hawakuwa na wasiwasi naye kama kuna jambo linalomsumbua.

Pia, alitumia fursa hiyo kuwaeleza mashabiki wake kuwa yupo vizuri na kuwaomba waendelee kumuunga mkono katika kazi zake.

Source:Mwananchi

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW