Burudani

Rihanna awaita Drake na Young Money ‘a**holes’

Inaonekana mvua ya habari za Rihanna haitaki kukatika. Baada tu ya kusababisha bonge la issue kwa kumbusu mpenzi wake wa zamani, Chris Brown, sasa limeibuka lingine kubwa.

Wakati Drake na timu yake ya Young Money ilipopanda juzi jukwaani kwenye za MTV VMA’s kupokea tuzo ya Best Hip Hop video, camera zilizoom sura ya Rihanna na kumkuta akiongea maneno yaliyotafsirika kama “I hate these a**holes.”

Kuna tetesi pia kuwa Rihanna na Nicki Minaj walitupiana maneno kwenye tuzo hizo.

Hata hivyo baada tu ya show hiyo Rihanna alichukua private jet na kuelekea jijini London kwenye mambo yake.

Rihanna, Jay-Z na kundi la Coldplay watatumbuiza kwenye ufungwaji wa mashindano ya Paralympics.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents