Burudani

Rihanna kuwa star kwenye reality show ya Uingereza


Hatimaye mwanadada Rihanna ameamua kuingia kwenye ulimwengu wa reality show. Kwa muda mrefu kulikuwa na fununu kuwa Rihanna angekuwa ‘host’ wa reality show ya mambo ya fashion, lakini sasa imejulikana rasmi.
Ri-Ri amesainishwa kama mtayarishaji mkuu na kuonekana kwenye shindano jipya la mitindo, “Styled to Rock,” ambalo litarushwa na kituo cha runinga cha Uingereza cha Sky Living HD kwa wiki nane mwezi ujao.
“Siku zote ninapenda fashion,” mzaliwa huyo wa Barbados, anasikika akisema kwenye ‘teaser trailer’ ya kipindi hicho kipya.”Fashion imenisaidia kujitengeneza kuwa msanii nilivyo hivi leo.”
Kutokana na kipindi hicho Rihanna atalazimika kuhamia nchini Uingereza kwa muda kwa ajili ya maandalizi na pia kuwafundisha wabunifu wa mitindo wachanga wa nchini Uingereza kufanikiwa zaidi.
Rihanna ataambatana na stylist wake Lisa Cooper, fashion designer wake Henry Holland na Nicola Roberts wa kundi la pop la Girls Aloud.
Katika shindano la mwisho la series hiyo washiriki watatakiwa kubuni vazi ambalo Rihanna atalitumia kuperfome kwenye show zake za live.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents