Habari

RIPOTI: Hawa ndio wafanyakazi wa BBC wanaolipwa hela nyingi zaidi

Chris Evans amekuwa wa kwanza katika orodha ya wafanyakazi nyota wa BBC wanaolipwa mishahara ya juu zaidi.


Chris Evans

Alilipwa kati ya pauni milioni 2.2 na milioni 2.25 mwaka 2016/2017, huku Claudia Winkleman akiwa mwanamke mfanyakazi nyota wa BBC anayelipwa mshahara wa juu zaidi, akiwa anapiliwa kati ya pauni 450,000 na 500,000.

Karibu theluthi mbili ya nyota wanaolipwa zaidi ya pauni 150,000 ni wanaume ikilinganishwa na theluthi moja ya wanawake.

Mkurugenzi mkuu wa BBC Tony Hall alisema kuwa kuna mengi yanahitaji kufanywa kwa suala ya jinsia.
Viwango ambavyo vimetolewa katika ripoti ya kila mwaka ya BBC, vinafichukua mwanya wa malipo ulio kati ya wanawake na wanaume.

Kwa ujumla wanaume25 wanaofaya kazi inayohitaji vipawa, hulipwa zaidi ya pauni 250,000 ikilinganishwa na wanawake tisa tu.

Hii ndiyo mara ya kwanza mishahara ya wafanyakazi nyota wa BBC wanaolipwa zaidi ya pauni 150,000 imetangazwa kwa umma.

Ripoti hiyo ya kila mwaka hata hivyo haijatoa kiwango kamili cha mishahara na pia haijajumuisha wafanyakazi nyota ambao hupokea mishahara kutoka BBC Worldwide.

Pia orodha hiyo haikutofautisha mishahara ya watu wanaofanya kazi zaidi ya moja ndani ya BBC na wale walio na kazi moja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents