DStv Inogilee!

Ronaldo aliamsha dude Italia, akamilisha ahadi ya kocha wake ya kusafisha nyota

Mshambuliaji wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, amefunga mabao yake mawili ya kwanza kunako ligi kuu ya soka nchini Italia (Serie A) ikiwa ni mabao yake ya kwanza kwenye mechi 4 alizoichezea Juventus.

Cristiano Ronaldo

Ronaldo amefunga mabao hayo kunako dakika ya 50 na 65, hivyo kuipa ushindi timu yake ya Juventus wa mabao 2-1 dhidi ya Sassuolo, ambao bao lao limefungwa na Khouma Babacar dakika ya 90.

Kwa matokeo hayo, Ronaldo atakuwa amekamilisha ahadi ya kocha wake, Massimiliano Allegri ambaye juzi Ijumaa aliahidi kuwa Ronaldo wiki hii itakuwa ni yake na ataanza kufunga magoli.

Allegri aliahidi hayo kwenye mazoezi mjini Turin baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kuhusu ukame wa magoli kwa mchezaji huyo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW