Michezo

Ronaldo arejea kwa mkosi La Liga: Madrid wanyukwa na Betis (+video)

Klabu ya Real Madrid imeonja joto ya jiwe baada ya kukubali kipigo cha goli 1-0 nyumbani kwao dhidi ya Real Betis.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa kwanza wa La Liga kwa mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo kuitumikia klabu yake baada ya kufungiwa mechi tano za Ligi mapema mwanzoni mwa msimu huu kwa kitendo cha kumsukuma mwamuzi kwenye fainali ya Super Cup.

Goli la Real Betis limefungwa kunako dakika za majeruhi (90+) za mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji wake, Antonio Sanabria.

Kwa sasa klabu ya Real Madrid ipo nafasi ya 7 kwenye msimamo wa La Liga wakiwa na pointi 8 huku wapinzani wao Barcelona wakiongoza Ligi kwa pointi 15. Tazama jinsi Madrid walivyochabangwa

https://youtu.be/PHqCCjkaXp4

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents