Habari

Rota MC na Charles Karume ndio wafalme wa Str8 Music Free Style

Jaji Dj AD aka Mafuvu
Washiriki Rota na Charles Karume Jumamosi usiku waliibuka washindi wa jumla wa mitindo huru kwa Rota na Charles Karume kuwa mfalme wa ku Dj katika mpambano mkali na wa kuvutia wa Str8 Music Free Style and Dj Competition 2012.

Shindano hilo ambalo lilifikia tamati baada ya jumla ya wasanii wa mitindo huru 8 pamoja na ma Dj 6 kuchuana vikali ili kuwapata washindi wa jumla kwa mwaka 2012 ambapo shindano hilo lilianzia katika hatua ya robo fainali.

Ilichukua masaa takribani 7 toka kuanza kwa shindano hadi kumalizika kwani shughuli ilibidi muda mwingine isimame ili kurekebisha vifaa vya muziki ili majaji wafanye kazi kwa fair play maana ilionekana vinawakwamisha washiriki.

Majaji wa shindano hilo ambao walikuwa pamoja na aliyewahi kuwa msanii na mtangazaji wa East Africa TV Saigon, prodyuza maarufu Dunga na kwa upande wa ma Dj waliongozwa na Dj Nelly kutoka Clouds Fm pamoja na Dj AD Mafuvu kutoka East Africa waliwatangaza Rota MC kama mshindi wa shindano ya mitindo huru, pamoja na Charles Karume kutawazwa kuwa mshindi wa taji la Dj Mfalme kwa mwaka 2012.

Aidha katika fainali hizo kazi haikuwa ngumu kuamua mshindi ilipofika fainali kwani Rota MC alifanya kile ambacho mashabiki hawakukitarajia kwa kumwaga mashairi makali dhidi ya mpinzani wake Mo Mnyama ambaye hakuweza kujibu mapigo na kuonekana dhahiri kuwa taji limeenda kwake, ambapo hata mashabiki walikuwa wanamkubali ile mbaya .

Katika upande wa Ma Dj hapo napo dalili za ushindani kati ya Charles Karume na Ally B zilianza kuonekana tangu awali kwani wawili hao walionyesha uwezo wa hali ya juu katika kumiliki mashine, uchaguzi wa nyimbo, kucheza na mashabiki, kusugua ama ku scratch na kumix nyimbo.

Utamu ulikolea pale ilipofika fainali ambapo washiriki hao wawili walipambana katika mizunguko miwili ambapo washindani hao walitakiwa kutumia mashine hizo kwa dakika tatu na kuhamia nyingine na kupiga kwa dakika tatu nyingine. Charles Karume alianza na ally B akajibu katika raundi ya kwanza. Kimbembe kikawa roundi ya pili ambapo Charles alianza na kuonyesha uwezo wa hali ya juu ambao ulipelekea Dj Ally B kumgwaya na kumpa ushindi kwa kutangaza yeye mwenyewe mbele ya hadhara kuwa amekubali Dj Charles apewe ushindi.

Katika fainali hizo za Str8 Music Free Style and Dj Competition 2012 zilizofanyika katika Club ya usiku ya San siro iliyopo maeneo ya Sinza jijini Dar-es-Salaam makundi ya Breakdance yalishindanishwa ambapo kundi la Best friend liliibuka na ushindi dhidi ya kundi la B Boys na kufanikiwa kujizolea zawadi ya shilingi milioni moja.

Mshindi wa str8 music freestyle Rota alijishindia mkataba wa kurekodi nyimbo tatu pamoja na promosheni, na mshindi wa Dj competition Charles Karume alijishindia mashine mpya kabisa ya kupigia muziki aina ya Pioneer na spika za kichwani za Beats by Dre ambazo zimekuwa maarufu sana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents