DStv Inogilee!

Ruby aliondoka King Empire baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu – Shetta

Msanii wa muziki Shetta ambaye ni mmoja kati ya viongozi wa label ya King Empire ambayo inawasimamia wasanii kama Aslay, The Mafik na wengine wengi amefunguka kueleza sababu ya muimbaji Ruby kuachana label hiyo.

Hapo awali taarifa zilidai kwamba muimbaji huyo aliondoka kwenye label hiyo baada ya kupishana kauli na Shetta ambaye ameachia video ya wimbo Hatufanani akiwa amewashikirikisha Jux na Mr Blue.

Akizungumza na Clouds FM wiki hii Shetta amesema Ruby alisimamisha na label hiyo baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu.

“Siwezi kusema sababu bali sisi ni familia kuna vitu vinatokea hata wachawi hugombana usiku wakiwanga, Hivyo kulitokea mpishano wa kauli kati yake na Meneja Kapasta kwenye group hivyo nikamwambia Ruby muheshimu kiongozi mara akanivamia na mimi hivyo nikamwambia #hambuso aandike barua ya kumsimamisha kwa muda kwa utovu wa nidhamu na angerudi tungezungumza lakini naona akaamua kufanya kazi zake yeye kama yeye,” alisema Shetta.

Mwezi mmoja uliopita muimbaji Vanessa pamoja na wadau wengine kupitia mitandao ya kijamii walikuwa wanamsifu binti huyo kwa uwezo wa kuimba huku wakimshauri akiacha kiburi atafika mbali kwenye muziki wake.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW