Habari

Run-DMC kurejea kwenye stage tangu muongo mmoja uliopita


Kundi kongwe la hip-hop nchini Marekani maarufu kama Run-DMC halijawaji kutumbuiza pamoja kwa muongo mmoja sasa. Lakini kwa sasa wahusika wa kundi hilo wanajiandaa kuunagana kwa mara nyingine tena na kudondosha makamuzi kwenye tamasha la Fun Fun Fun Fest jijini Austin, Texas.
Joseph Simmons, maarufu kama Rev. Run, na Darryl “DMC” McDaniels walistaafu wakiwa na kundi hilo baada ya DJ wao Jam Master Jay, kuuawa mwaka 2002.
Lakini jana imetangazwa kuwa kundi hilo litakuwa miongoni mwa watumbuizaji kwenye tamasha hilo litakalofanyika November 2-4, mwaka huu.
Waandaji wa tamasha hilo wamesema wana mpango wa kuchangia baadhi ya mapato yake kwa taasisi ya JMJ Foundation for Music, ambayo huwasaidia vijana katika masuala ya sanaa.
Kundi la Run-DMC lilitamba sana na vibao kama “Walk This Way,” “It’s Like That” na “My Adidas.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents