Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Safari ya Happiness Millen Magese kuwapa moyo wanawake

Hii ni ndoto ya kila mwanamke kuitwa mama. Hapa tumepata somo kwa aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2001 Millen Magese, ambaye amefanikiwa kupata mtoto wake wa kwanza wakiume Kairo, siku ya Julai 13 mwaka huu.

Millen ambaye ni mwanamitindo alijitangaza hadharani kuwa na tatizo linalofahamika kitaalam kama Endometriosis,tatizo ambalo huwakuta wanawake wengi pindi wanapoingia hedhi na hupeleka kutokuwa na uwezo wa kushika ujauzo.

Millen anaweza kuwa dira kwa wanawake ambao walishakata tamaa ya kupata mtoto, kwa kuwa wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hilo. Tumeona somo jingine kuwa hakuna wa kubishana na Mungu kwani yeye ndio anajua kesho yetu.

Hii ni faraja kubwa kuona muanzisha taasisi hiyo akipata mafanikio katika harakati zake za kutoa elimu hususani kwa Watanzania ambao wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huo na sasa watapata kujua nini cha kufanaya.

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW