Habari

SBL yakabidhi mradi wa maji kwa wakazi 12,000 wa Kabila Magu

Kampuni ya Bia Serengeti na shirika lisilola kiserikali, African Community Advancement Initiative (AFRIcai) wamezindua  mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 215  katika Kijiji cha Kabila wilayani Magu mkoaniMwanza ikiwa ni jitihada za kuwapelekea maji safi na salama wananchi wa eneo hilo.

Ukiwa na uwezo kwa  kuhudumia wakazi 12,000 mradi huo unahusisha ufungaji wa pampu ya kuzamisha ndani ya kisima, ujenzi wa nyumba ya pampu, tanki la kuhifadhi maji, mtandao wamabomba ya maji, na vituo vipya vya maji 13 vyenye uwezo wakutoa mita za ujazo 87,000 za maji kwa mwaka.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, aliwapongeza SBL na AFRIcai kwa kutoa msaadamuhimu kwa wakazi wa Kijiji cha Kabila, alinukuliwa, ‘‘mashirika haya binafsi yamekuwa mstari wa mbele katikakukuza miradi ya maendeleo nchini ambayo inawezesha kuwepokwa jamii iliyo na uzalishaji na afya bora. Mtanda aliongeza, ‘‘Ushirikiano kati ya SBL na AFRIcai unathibitisha dhamira yasekta binafsi kwa uwajibikaji wa kijamii na maendeleo endelevu. Kwa kuwekeza katika miradi inayolenga mahitaji msingi ya jamiikama usambazaji wa maji, SBL na AFRIcai wanadhihirishadhamira yao ya kuboresha ustawi wa jamii ya watanzania nakuchochea mafanikio ya muda mrefu.”

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji waSBL, Obinna Anyalebechi alisema kuwa mradi huo ambao unajulikana, Water for Life (Maji kwa ajili ya uhai) ni miongoni mwa mikakati ambayo kampuni hiyo ya bia inaendesha katika mikoa ya Iringa, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Mwanza, Singida, Mara, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwa imewanufaisha zaidi ya watu milioni mbili kwa maji safi na salama.

Mwaka huu, Serengeti Breweries Limited (SBL), kwakushirikiana na African Community Advancement Initiative (AFRIcai), tumekamilisha ujenzi wa mradi huu muhimu wa majikatika kata ya Kabila, Wilaya ya Magu, Mkoa wa Mwanza. Kwa kutambua kwamba maji ni hitaji la msingi la maisha na moja yarasilimali muhimu zaidi, SBL kupitia mpango wake wa kusaidiajamii, imekuwa ikitekeleza miradi ya maji katika maeneombalimbali ya nchi kwa lengo la kutoa maji bure kwa watuwanaoishi katika maeneo yenye uhaba mkubwa wa maji nchini. Kupitia sera ya Water fo Life hadi sasa tumetekeleza miradi 26 yamaji katika maeneo yenye uhaba wa maji katika sehemumbalimbali za nchi, ambapo zaidi ya watu milioni 2 wamenufaikana miradi hii ambayo inalenga kutoa maji safi na salama.”

Nae Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu wa SBL, RispaHatibu alisema, “Mradi wa Kabila sio tu kwamba utaboresha afya za wakazi wa eneo hilo bali pia utaongeza tija kiuchumi hususani kwa watoto wa kike na wanawake ambao hawatahitaji kutumia saa nyingi kutafuta maji safi na salama sehemu nyingine. Hii inawapa fursa ya kuhudhuria shule  wakiwa huru.

Akihutubia katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikalisilo la Kiserikali la African Community Advancement Initiative (AFRIcai) Bonus Caesar aliongezea kwa kusema kuwa shirikahilo lina sera zilizojikita katika ustawi wa jamii katika maeneo yamaji, afya, elimu na uwezeshaji.  

Caesar alisemaUshirikiano huu wa kimkakati baina ya SBL naAFRIcai unalenga kuondoa uhaba wa maji kwa kuwapatia majisafi na salama wananchi 11,927 katika vitongoji vya Ilambu, Mlimani, Igogo, Shuleni na Majengo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents