Sean Kingston, Romeo na familia zao waanzisha Reality TV Show
Muimbaji wa ‘Beautiful Girls’ Sean Kingston na rapper Romeo Miller pamoja na familia zao wameanzisha Reality TV show yao iitwayo Fame in the Family.
Show hiyo itakayoanza kuruka February 17 kupitia kituo cha runinga cha E! itaonesha maisha ya wasanii hao pamoja na familia zao.