Senzo ajieleze, tumepokea kwa mshtuko uamuzi wake – Simba yatoa tamko

Klabu ya Simba imekiri kupokea kwa mshtuko uamuzi wa kujiuzulu kwa Senzo Mazingiza na kumtaka ajieleze mambo ambayo hayajakamilika na kufanya makabidhiano kwa weledi haraka iwezekanavyo.

”Klabu ya Simba imepokea kwa mshtuko uamuzi wa kujiuzulu kwa Bwana Senzo Mbatha Mazingiza. Kwa niaba ya Klabu, tunaandika kuwajulisha umma kwamba Klabu haitahusika na jambo lolote linalohusiana na Simba ambalo Bwana Senzo atafanya kuanzia sasa.”- Simba SC

‘Bodi ya Klabu ya Simba imemtaka ajieleze kuhusu, mambo ambayo hayajakamilika na kufanya makabidhiano kwa weledi haraka iwezekanavyo.”

”Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, tunawashukuru wote kwa utulivu huku tukisubiri kutanga Kaimu Ofisi Mtendaji Mkuu katika siku kadhaa zinazokuja.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW