Burudani

Serikali ibadili jina la Miss Tanzania – Afande Sele

Baadhi ya wadau akiwemo msanii mkongwe wa muziki nchini kutoka Morogoro, Afande Sele ameonyesha kutoridhishwa na zawadi ya gari aliyopewa Miss Tanzania 2016/17, Diana Edward kwa madai limechakaa na linashusha hadhi ya mashindano hayo nchini.

Afande Sele

Rapa huyo ameishauri wizara husika kubadili jina la shindano hilo kwa madai wanalitia aibu Taifa.

“Utapeli ni nini?. Gari ya Miss Tanzania 2017 na gari ya Miss Tanzania 2011 zinatoa jibu la swali hilo,” aliandika Afande Sele Intagram. “Lakini pia ni vyema tukamuomba waziri husika katika masuala hayo akamuulize muandaaji wa Miss Tanzania kama ni kweli ameamua kuzeeka labda hata kufa na shindano lake?,”

Aliongeza, “Na kama kweli iko hivyo basi itoshe pia kubadili jina la shindano kwa kuliita miss jina lake badala ya kuendelea kutia aibu faifa kwa kuliita Miss Tanzania huku likikosa hadhi ya kitaifa katika maeneo yote kwa makusudi na maslahi yake yeye mtu mmoja tu. Aibu yake aibu yetu. Imetosha sasa, imetosha sana,”

Miss huyo alikabidhiwa gari hilo wiki iliyopita baada ya kusubiri kwa zaidi ya miezi sita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents