Habari

Serikali ikubali kusikia mazuri na mabaya – Mkurugenzi LHRC

Mkurugenzi wa sheria na kituo cha haki za binadamu,LHRC, Dk Hellen Kijo Bisimba ameitaka serikali kukubali kusikia mazuri na mabaya na kuyatumia maoni ya wananchi ili kuwapatia Watanzania maendeleo endelevu.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Bisimba wakati akitoa tamko la kituo hicho baada ya vituo vitano vya runinga kupigwa faini kwa kile kilichoelezwa kuwa ukiukwaji wa maudhui.

“Tumeshuhudia serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)ikitoa adhabu kwa vituo vikuu vitano vya runinga ikiwemo, Azam Tv, ITV, Channel 10, Star Tv, EATV kwa kile kinacho daiwa ni ukiukwaji wa kanuni za maudhui ya mwaka 2015 baada ya Televisheni hizo kurusha habari kuhusu tathmini ya haki za binadam katika uchaguzi mdogo wa madiwani na tathimini hiyo ilitolewa na Kituo cha sheria na haki za binadamu kwa mujibu wa Kamati hiyo ya maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini vyombo hivyo vimetiwa hatiani kwa makosa matatu chini ya kifungu cha 5 na cha 6,“ amesema Bisimba.

“Serikali kupitia jeshi la polisi wamekuwa wakitumia neno uchochezi kuminya uhuru wa mawazo na uhuru wa kujieleza kutumika kwa mamlaka nyingine za serikali kuminya uhuru wa kujieleza hivi karibuni tumeshuhudia mamlaka ya mapato TRA ikijiingiza katika Malumbano na Askofu wa Full gospel, Askofu Kakobe kwa kile tu alichokisema madhabahuni kama sehemu ya mahubiri kwenye ibada kanisani.“

“Serikali ikubali kusikia mazuri na mabaya na kuyatumia maoni ya wanachi ya wananchi wake katika kuwapatia Watanzania maendeleo endelevu, “ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents