Habari

Serikali kuchukua hatua kali kwa waharibifu wa Mazingira

Serikali Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira imeeleza njia mbalimbali za kukabiliana na uharibifu wa Mazingira ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaokamatwa wakikata miti bila vibali kwa mujibu wa sheria.

Hayo yamezungumzwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Muungano na Mazingira,Luhaga Mpina wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Faharia Shomari Khamis lililohoji

Uharibifu wa Mazingira nchini unaleta athari kubwa ya mabadiliko ya msitu wa kilimo, uhaba mkubwa wa maji na kukauka kwa vyanzo vya maji, Je? Serikali imechukua hatua gani za makusudi za kudhibiti uharibifu huo?

“Katika kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira zinazolikabili Taifa hili, Serikali imechukua hatua zifuatazo kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaokamatwa wakikata miti bila vibali kwa mujibu wa sheria, kutoa elimu ya mazingira kwa umma ili kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira hasa misitu,”alisema Mhe. Mpina.

“Kuhamasisha wananchi kutumia nishati mbadala kama gesi na umeme pamoja na matumizi ya majiko banifu ili kupunguza matumizi ya mkaa na kuni.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents