Habari

Serikali kuingilia kati suala la wasichana kupelekwa nje kufanya biashara ya ngono

Serikali imesema wajibu wake kuhakikisha Watanzania wanaopata fursa ya kufanya kazi nje ya mipaka ya Tanzania wanafanya kazi katika Mazingira mazuri na yanayolinda staha na utu wao.

Serikali imesema kama kuna wasichana wanapelekwa nje ya nchi yakufanya biashara ya ngono ikijulikana haitasita kuchukua hatua kali dhidi ya wanaofanya hivyo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Suzan Kolimba ametoa ufafanuzi huo, leo Mei 21 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge, Hawa Mchafu aliyeuliza,

Je ni hatua gani kali zinazochukuliwa dhidi ya wafanya biashara wanaosafirisha vijana wa Kitanzania hususani vijana wa kike kwenda nje ya nchi kwaajili ya kufanya biashara isiyo rasmi ikiwemo kuuza miili yao.? Ni ipi sasa kauli ya serikali dhidi ya madai ya kusikitisha sana kuwa baadhi ya Watanzania wanasafirishwa kwenda nje wanaenda kuuzwa figo zao?

“Kuhusu hatua gani kali zimechukuliwa kuhusu wafanya biashara ambao wamewapeleka wasichana nje kwenda kufanya biashara ya kuuza miili yao kwa kweli niseme kwamba hiyo ikijulikana hatua kali za nchi yetu zitachukuliwa lakini so far mimi sina data za aina hiyo,” amesema Dkt. Kolimba.

“Lakini kuhusu kwamba kuna Watanzania ambao wamepelekwa nje na kwamba wanapopelekwa nje figo zinachukuliwa hilo pia sisi tutafuatilia kama kuna ukweli hatua kali zitachukuliwa kwenye nchi husika.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents