Habari

Serikali kuja na mpango wa kodi ya nyumba kulipwa mwezi mmoja mmoja

Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema kuwa iko kwenye mchakato wa kuanzisha mamlaka itakayo simamia masuala ya kodi ya nyumba itakayo fanya ukomo wa kodi kulipwa kwa mwezi mmoja na si miezi sita wala kumi na mbili.

Hayo yamezungumzwa leo bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Angelina Mabula wakati akijibu swali la Mbunge Halima Bulembo aliyehoji

Je, ni lini sasa serikali itafuta utaratibu wa kulipa kodi kwa miezi 6 au mwaka sambamba na kuomba bunge kutunga sheria itakayo walazimisha wamiliki wote kupokea kodi kwa mwezi mmoja badala ya kulipa kama ilivyo sasa?

“Naomba nimtaarifu Mhe. Mbunge pamoja na wabunge wizara tayari imekwisha liona hilo, na tayari tuko kwenye mchakato wa kuanzisha mamlaka itakayo simamia masuala yote ya nyumba na katika sheria, na hiyo sheria italetwa hapa bungeni. Tumeangalia suala la ukomo wa kutoa kodi za nyumba hiyo ya miezi sita na mwaka mmoja haita kuwepo,amesema Mabula.

“Tumeona inaumiza watu wengi kwahiyo kodi itakuwa inalipwa kwa mwezi mmoja mmoja na wakati huo huo utatakiwa kuweka kama amana ya miezi mitatu kwaajili ya shughuli zingine ambazo zinaweza kuwa, kwahiyo suala hilo limelisikia na tunalifanyia kazi ,” amesema Mabula.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents