Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Serikali kuwashughulikia waharibifu wa miundombinu

Serikali imesema kuwa waoihujumu miundo mbinu kwa kuiharibu hawatasita kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwasababu serikali inatumia fedha nyingi kuboresha miundombinu hiyo.

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa amezungumza hayo leo, Mei 17 Bungeni Jjini Dodoma, wakati wa Kipindi cha Maswali ya PAPO kwa PAPO ambapo amesema kuwa kila Mtanzania anajukumu na kulinda miundombinu.

“Serikali inatumia fedha nyingi sana kwaajili ya kuboresha miundo mbinu, Miundombinu hii tunawajibu wa kuilinda Watanzania na endapo atatokea mtu miongoni mwa Watanzania wenye nia mbaya wanaihujumu miundombinu hii serikali hatuwezi kukaa kimya lazima tuchukue hatua,” amesema Waziri Mkuu.

Aidha Waziri Mkuu ameongeza kuwa jukumu la serikali ni jukumu la Watanzania wote na kila Mtanzania ana dhamana ya kulinda ulinzi na usalama wa ndani ya nchi ikiwa ni pamoja na kulinda miundo mbinu ya nchi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW