Habari

Serikali ya Zanzibar yapiga marufuku siasa katika nyumba za ibada

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepiga marufuku wanasiasa kutumia nyumba za ibaada kufanya kwa shughuli za kisiasa.

mohamed-aboud

Tamko hilo limetolewa na waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais wa Zanzibar, Mh. Mohammed Aboud alisema kuwa viongozi wa dini na kamati zao katika nyumba za ibada watakaoruhusu wanasiasa kuendesha shughuli hizo, watawajibika kwa mujibu wa sheria za nchi .

“Ninatoa hoja ya kuzungumza nanyi kupitia taarifa hii kwa lengo la kuelimisha na kuwatahadharisha kwa mwenendo wa baadhi ya viongozi wa kisiasa kutumia nyumba za ibada hususani misikiti, kuwa ni majukwaa ya kisiasa kwani jambo hilo ni hatari sana kwa mustakabali wa Zanzibar, Tanzania na wananchi kwa ujumla,” alionya Aboud.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents