Habari

Serikali yapiga marufuku kununua vitoweo kutoka nje ya nchi

Serikali imepiga marufuku kuagiza na kuingiza nyama za kuku waliochinjwa kutoka nje ya nchi ili kulinda afya za walaji wa bidhaa hiyo ya nyama nchini.


Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha.

Marufuku hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha kwenye mahojiano maalum na kituo cha EATV, ilipotaka kupewa ufafanuzi wa serikali kuwa inahakikisha vipi nyama na vitoweo kutoka nje ya nchi zinaingizwa nchini zikiwa na ubora unaokidhi viwango vya afya kwa walaji.

Naibu waziri huyo alisema hairuhusiwi kuagiza wala kuuza kuku waliochinjwa kutoka nje ya nchi kwakuwa kwa sasa nchi inajitosheleza na inajitegemea kwa kiwango kikubwa cha nyama. Aidha aliwataka wafugaji na wafanyabiashara kutumia fursa za kuzalisha nyama kwa tija na ubora zaidi ili nchi ianze kuuza vitoweo vya nyama hasa kuku nje ya nchi.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents