Shaa aja na mikakati mipya ya kwenda ‘international’ ashoot video ya ‘LavaLava’

Pamoja na kuachia video na wimbo wa Promise, Sarah Kaisi aka Shaa haoneshi dalili za kupumzika. Infact, mwaka huu amedhamiria kusogea mbele zaidi kwa kuupeleka muziki wake kimataifa.

62105_10151485745518570_874029548_n

Hivi karibuni alikuwa busy kufanya rehearsal na kushoot video ya ngoma yake iitwayo Lava Lava ambayo inaongozwa na Adam Juma wa Visual Lab. Akiongea kwenye Exclusive Friday ya Times FM leo, Shaa amesema amefanya video hiyo kutokana na kuwa na malengo ya kuvuka mipaka.

“Malengo yangu ni kuangalia kuvuka mipaka, kwahiyo ni video ambayo obvious nataka ivuke mipaka lakini sio kwamba hapa nyumbani hawataiona, kwa wale ambao wana ving’amuzi, kwa wale ambao ni wajanja katika internet, wataiona tu,” alisema Shaa.

Kila lakheri Shaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents