Burudani

Shaa anahisi Ben Affleck ana mtihani mgumu kucheza vizuri uhusika wa Batman

Sarah Kaisi aka Shaa ni miongoni mwa mamilioni ya mashabiki wa filamu duniani walio na wasiwasi kuhusu kama Ben Affleck anaweza kuigiza vizuri filamu ya Batman.

NEaPJCgNU12adg_1_2

Kupitia Twitter, Shaa ambaye hivi karibuni ataachia wimbo wake mpya, Sugua Gaga, amesema kuwa baada ya kuangalia upya filamu za Batman zilizopita, anahisi Ben atakuwa na wakati mgumu.

“After watching the Batman movies re-runs over the weekend….Ben Affleck ana-ka mtihani wallahi,”alitweet.

Mashabiki wa filamu duniani walipinga vikali uamuzi wa kampuni Warner Bros. Kumchagua Ben Affleck kwenye filamu ijayo ya Batman, Batman vs. Superman ambapo zaidi ya petitions 30 zilitumwa kwenye mtandao wa Change.com kutaka aondolewe.

“Uwezo wake wa kuigiza haukaribiani hata kidogo kuaminika kuwa kama Bruce Wayne na hatoweza kuitendea haki nafasi hiyo,” ilisomeka petition moja iliyokuwa na sahihi 3,200. Nyingine ilisainiwa na 6,000.

“Hajajengwa, na wala hashtushi vya kutosha kwa uhusika wa Batman.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents