Burudani

Shamsa Ford atoa funzo kwa mastaa wa kike wanaochagua wanaume wa kuoa

By  | 

Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Shamsa Ford amefunguka kwa kuwaonya Mastaa wa Wanawake waache tabia za kuchagua wanaume wa kuwaoa, kwani leo wana majina makubwa na wanaonekana warembo lakini ipo siku itafika hata hao wanaume wanaowatongoza leo watapotea kabisa.

Tokeo la picha la shamsaford

Muigizaji ‘Shamsa Ford’

Shamsa Ford amesema kwa sasa Wanawake wenye majina makubwa wanajiona warembo kiasi kwamba hufikia hatua hata ya kusubiri wanaume matajiri wa kuwaoa bila kukumbuka kuwa hata hao matajiri wana watu wao huku wakisahau kuwa ndoa ni baraka toka kwa Mungu na ina heshima kubwa sana.

Wasichana wenzangu maisha ni mafupi sana leo tunavuma na kupendwa kila kona tunapokatiza ila kuna muda utafika hata nzi hakusogelei.Hata uwe mzuri na maarufu kiasi gani lakini ndoa ina heshima yake.Msiwe wachaguzi sana.Maana ukisema unamsubili tajiri aje akuoe na yeye huyo tajiri ana mwanamke wake aliyetoka naye mbali kimaisha.“Ameandika Mrembo Shamsa Ford kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akiwapa somo wanawake wenzie kuhusu Mwanaume wa kuoa

Cha muhimu ni kumuomba Mungu akupe mwanaume mwenye kumjua Mungu,mwenye upendo,heshima,mtafutaji hayo mengine yanakuja tu..Nguvu ya mmoja ni tofauti na ya wawili “Ameandika Shamsa Ford.

Shamsa Ford kwa sasa yupo kwenye ndoa na mfanyabiashara Chidi Mapenzi.

By Godfrey Mgallah

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments