Habari

Shemeji wa Dj Khaled auawa katika dili la madawa ya kulevya

Mdogo wake na mpenzi wa DJ Khaled amepigwa risasi na kufa katika nyumba iliopo Bronx, New york nchini marekani Jumapili usiku. Jonathan Tuck ambaye ndiye mdogo wa mpenzi wa DJ Khaled Nicole Tuck aliuawa baada ya mpango wa kuuziana madawa ya kulevya kwenda vibaya.

Jonathan alikuwa akijaribu kununua bangi na ghafla mtu alimsogelea na kummiminia risasi usoni majira ya saa tatu usiku siku ya Jumapili katika ghorofa moja iliopo Belmont ambayo haipo mbali sana na nyumbani kwake iliopo Bronx, kutokana na ripoti za NY Daily News. Alipelekwa Hospitali ya St. Barnabas ambako kwa bahati mbaya alikufa.

Polisi wa jiji la New York wanachunguza juu ya jambo lakini tukio hilo limefanyika baada ya kutoea mgongano katika dili hilo la kuuziana bangi. Polisi kwa sasa wanamshikilia wamechukua mtu mwenye umri wa miaka 34 kwa ajili ya kumhoji maswali, lakini bado hawajapata uhakika kama yeye ndiye muuaji.

Jonathan (kushoto) akiwa na rafiki yake[/caption]

Jonathan Tuck na dada yake walikuwa karibu, kulingana na rafiki yake wa zamani Brandon Davis. DJ Khaled alikuwa katika Minneapolis kwenye tamasha la Super Bowl wakati Tuck alipouawa.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents