Habari

Shujaa aliyepanda hadi ghorofa ya 15 Grenfell Tower kuokoa wahanga wa moto asimulia (Picha + Video)

Kijana, Leon Whitley ambaye ameonekana kama shujaa baada ya kuokoa maisha ya wahanga wa ajali ya moto iliyotokea hivi karibuni katika jengo la Grenfell Tower ameeleza namna alivyofika hadi ghorofa ya 15 katika kuwanusuru watu waliokuwa wamekwama katika ajali hiyo.

Shujaa,Leon Whitley  akiwa katika hali ya uzuni akisimulia namna alivuo yahatirisha maisha yake  kwaajili ya kuokoa watu  Grenfell Tower

Shujaa huyo ambaye aliyatoa maisha yake kwaajili ya kuokoa maisha ya watu wengine amesema alikuwa akisikia kelele za watu wakilia na kuomba msaada ndani ya moto huo uliozuka katika jengo Grenfell Tower

Zaidi ya watu 100 walihofia maisha yao baada ya milango kushinwa kufunguka mapema jumatano hii

Leon Whitley, mwenye umri wa miaka 34, alipanda mpaka katika ghorofa ya 15 ya jengo hilo licha ya moto mkali uliokuwa ukiendelea kuwaka huku akiliona tukio hilo kama lile lililotokea majengo pacha World Trade Center 9/11.

Leon akionekana kuwasili eneo la tukio nyakati za saa 1.45am  na kumuomba rafiki yake waongozane hadi ghorofa ya 15

Whiley ambaye kazi yake yupo katika kikosi cha zimamoto na uokoaji alisema.

“Nilisikia mtu akisema kama kunamtu yeyote wakuingia ndani amsaidie mwanangu na hicho ndicho nilichoamua kufanya.”

“Kilakitu huenda unapokuwa eneo la tukio, sote tunatambua namna lilejengo lilivyoweza kulipuka, mara zote hufanya kazi hii bila ya kuhofia lakini huu ndio moto wa kwanza nilio uwogopa.

“Kwanza unafikiria familia yako na namna unavyoipenda kabla ya kuanza kazi, kisha unaona sawa wacha utimize majukumu ya kusaidia watu.” Leon Whitley alikiambia chambo cha habari cha The Sun.

Leon aliwasili katika eneo la tukio West London nyakati za saa 1.45am na kisha kumuomba rafiki yake waongozane kwenda ghorofa ya 15. Watu zaidi ya 12 walithibitishwa kufariki kwenye tukio hilo.

BY HAMZA FUMO

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents