Habari

Shule 10 bora zilizoongoza kitaifa matokeo ya darasa la 7

Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), limetangaza matokeo ya  wa darasa la saba leo ambapo shule bora zilizofanya vizuri kitaifa ambazo ni kama zifuatazo St. Peters – Kagera, St Severine – Kagera, Alliance – MwanzaSir. John – Tanga Palikas – Shinyanga Mwanga – Kagera Hazina – Dar es salaam St. Anne Marie – Dar es salaam Rweikiza – Kagera Martin Luther – Dodoma.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 341,020 ambao ni sawa na asilimia 70.93 na wavulana ni 321,015 sawa na asilimia 74.80 .

Sambamba na matokeo hayo pia Dkt. Msonde ametaja ambapo Mikoa 10 iliyoongoza kitaifa ni mkoa wa Dar es salaam , Geita, Kagera, Iringa, Kilimanjaro, Njombe, Arusha, Mwanza, Katavi, Tabora.

Shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa ambazo ni Nyahaa – Singida, Bosha – Tanga, Ntalasha – Tabora, Kishangazi – Tanga, Mntamba – Singida, Ikolo – Singida,Kamwala – Songwe, Kibutuka – Lindi, Mkulumanzi – Tanga, Kitwai A – Manyara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents