Burudani

Shyrose avutiwa na Hip hop darasa la Fid Q, aahidi kuwatembelea.



Rapper Fareed Kubanda aka Fid Q ameendelea kupata heshima kutoka kwa watu wa aina mbalimbali kutokana na jitihada anazozifanya katika kukuza utamaduni wa hip hop nchini.
Hivi karibuni mashairi yake yalimvutia mhadhari wa chuo kikuu cha St. Augustine na sasa darasa lake la hip hop ambalo hufanyika kila weekend jijini Dar es Salaam limemvutia mwanasiasa kijana anayekuja kwa kasi nchini, mbunge wa Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji.
Baada ya kuvutiwa na maelezo aliyopewa na Fid kutokana na maswali aliyokuwa akimuuliza jana kupitia utaratibu wake wa kila siku za weekend wa AskFidQ, Shyrose amempongeza kwa jambo hilo na pia ameahidi kulitembelea darasa hilo ili kujionea linavyofanyika.
Darasa hilo ambalo kikazi lina miezi mitatu tu na kuanza na wanafunzi 25, sasa hivi lina jumla ya wanafunzi 52, ambapo 34 ni watoto wa mtaani.
Katika maelezo hayo Fid amesema darasa hilo huwasaidia wanafunzi hao kujitambua zaidi, kuwafunua mawazo na kuwafanya waishi katika mstari unaoendana na maadili ya kitanzania.
“OMG 34 its a huge number, Hongera sana, Mungu atakuzidishia. Wamefaidikaje na darasa tangu kuanza kwake?’ aliuliza Shyrose ambapo Fid alijibu kuwa watoto hao hupata Exposure.
“Asante sana mheshimiwa.. Na pia naomba ujue tutafurahi sana ukitutembelea darasani,” alisema Ngosha huku mbunge huyo akijibu, “Tuko pamoja, ntakuja.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents