Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Burudani

Si Harmonize na Wolper pekee, hawa ni wasanii wengine watano waliowatumia wapenzi wao kwenye video

By  | 

KWA sasa Harmonize msanii kutoka lebo ya Diamond Platnumz WCB ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Niambie.

Katika video ya wimbo huu anaonekana mpenzi wake Jacqueline Wolper ambaye hapo awali kulikuwa na tetesi kuwa wamemwagana. Kitendo cha Wolper kuonekana katika video hiyo kimenifurahisha kwa kuwa kimezima zile tetesi.

Lakini kimenifanya kuzama ‘chimbo’ langu la kukuletea ‘list’ ya wasanii wa Bongo Fleva waliowahi kuwashirikisha wapenzi wao katika video za nyimbo zao.

1.Diamond Platnumz

Mama Tiffah (Zari) alionekana kwenye video ya wimbo wa ‘Utanipenda’ uliotoka mwaka juzi mwishoni, video hiyo ilifanyika hapa Bongo.
Pia kipindi Diamond yupo kwenye mahusiano na Wema Sepetu alimshrikisha mrembo huyo katika video ya wimbo wa ‘Moyo wangu.’

2.Barnaba

Mke wake mama Steven alionekana kwenye video ya wimbo wa ‘Wahalade’ uliotoka mwaka 2014 na kufanya vizuri sana. Lakini msanii huyo alikaririwa akisema msanii yeyote hatoweza ‘kumtumia’ mkewe katika video isipokuwa yeye tu.

3.Jux

Mpenzi wake Vanessa Mdee alionekana kwenye video ya wimbo wa Sisikii uliotoka mwaka 2014, na wamekuwa na ushirikiano mkubwa katika masuala ya video. Ukitazama vipande vya video vya vyuma ya pazia wakati Jux akishoot video ya wimbo wa ‘Nikuite Nani’ Vanessa anaonekana pia. Hii ilikuwa ni kabla ya kuja kuachia wimbo wao wa pamoja uitwao ‘Juu.’

4.Mabeste

Alimshirikisha mke wake ‘Lisa’ kwenye wimbo wake ‘Usiwe bubu’, pia mkewe aliwahi kuwa meneja wa kusimamia kazi zake. Mwaka juzi walifunga ndoa na Ijumaa hii wamepata mtoto wa pili.

5. Nuh Mziwanda

Wakati bado yupo katika mahusiano na Shilole alimshirikisha katika video ya wimbo wa ‘Msondo Ngoma’, Shilole anaonekana mwanzoni na mwisho wa video hiyo. Pia sauti ya Shilole iliweza kusikika katika wimbo huo, ila kwa sasa hawa si wapenzi tena kila mtu ana maisha yake.

By Peter Akaro
Contact: 0755 299595

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW