Habari

Si vitabu vyote vina makosa – Prof. Ndalichako

Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amewataka Wabunge wavute subira waiachie serikali ilishughulikie suala vitabu vyenye makosa kwa umakini unaotakiwa na muda unaotakiwa.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo, leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali mbunge Suzan Lyimo lililouliza,

Pamoja na kwamba kamati imeundwa na Muheshimiwa waziri wa Elimu lakini nimepita kwenye shule mbalimbali vitabu vilevile vyenye makosa ndivyo vinavyotumika, nilitegemea wizara ingevitoa waendelee kutumia vitabu vya zamani, Je? sasa hamuoni kwamba kuendelea kutumika kwa vitabu hivyo ni makosa na makubwa na mnapanda sumu katika katika watoto wetu ni lini sasa mtaviondoa vitabu hivyo?

“Serikali imeendelea kulifanyia kazi na niwaambie waheshimiwa wabunge kuwa kwasasa hivi wanafunzi wapo likizo kwahiyo suala la kusema wanaendelea kutumia vitabu kwasasa hivi wapo likizo, lakini niseme tu kwamba si vitabu vyote vina makosa kama ambavyo serikali ilikwisha sema,” alisema Ndalichako.

“Baada ya kamati za wataalamu kukamilisha maamuzi ya serikali yatawasilishwa kama ambavyo tayari muheshimiwa kiti chako kilikuwa kimeelekezwa kwahiyo waheshimiwa wabunge wavute subira waiachie serikali ifanye suala hili kwa umakini unaotakiwa na muda unaotakiwa.”

Hata hivyo Waziri Mkuu alipiga marufuku watu binafsi kuchapisha vitabu badala yake uchapaji huo usimamiwe na Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) ili kuthibiti ubora.

Serikali yapiga marufuku watu binafsi kuchapa vitabu vya kufundishia

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents