Habari

Sijaelewa tafsiri ya uongo kwangu iko wapi – Ruge Mutahaba

Mkurugenzi na mzalishaji wa vipindi waClouds Media Group, Ruge Mutahaba, ameijibu kauli iliyotolewa na Mkuu wa mkoa wa Dar Dar es salaam, Paul Makonda ya kuwa yeye ni muongo, na anafaa tu kuwa muandishi wa mashairi na nyimbo za mapenzi na ngonjera.

Ruge ametoa kauli hiyo leo katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na kituo hicho, ambapo walikuwa na kipindi cha ‘SHUKRANI’ kwa wasikilizaji wao na watu waliowahi kuwasaidia kupata misaada.

“Kila mtu ana mtazamo wake, na huwezi kulazimisha mtazamo wa mtu ubadilike. Inasikitisha sana kuona mtu anayesambaza haya mambo ni bosi wangu, Bosi wa mkoa wetu. Yeye akipiga mhuri kitu ndio imekaa hiyo, Yeye ana nguvu zote,” amesema Ruge.

“Sasa akisema hivyo mimi ni tapeli anataka kila mtu Dar es Salaam anione hivyo. Mimi sina nguvu kwa hiyo nachagua kubaki kwenye ninacho kiamini. Tangu mwanzo nilisema mimi nataka haya mambo yaishe, cha kusikitisha huyu mtu ni kiongozi lakini anashindwa kumaliza jambo hili kwa busara na anataka kuliendeleza.

“Kuna mambo hapa yanajaribu kutengenezwa. Watu wanajaribu kutusukuma turudi kwenye mjadala ambao tulishaumaliza. Mimi ni mtu mzima , na busara inaniambia watu wazima hatuna haja ya kurudi kwenye majibizano ambayo kwangu yaliisha siku nyingi “alieleza Ruge.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa Star Tv kwenye kipindi cha Tuongee Asubuhi amezungumzia suala la Kuvamia kituo cha Clouds Media hivi “Mambo yaliyoelezwa ndio yanayonisikitisha sana, Nimeuona uongo wa Ruge hadharani, nimeuona utapeli wake hadharani nimeisikitika sana kauli yake kwamba Yesu alifanya mambo mengi lakini kumbe tunaweza kugeukana sisi kwa sisi.”

“Nilijiuliza mawali mengi sana moja wapo nikawa nasema kama mimi nimekosea kwa mahusiano ambayo tunafahamiana, kwamba tumefikia kwenye kiwango hiki ndiyo maana hata simu zangu waligoma kupokea kulikuwa na agenda gani Ok, ni kosa langu la ngapi Je walishindwa hata kumtafuta kiongozi wangu hata mmoja kumwambia kwamba hatujafurahishwa na mpendwa wetu ndugu yetu ambaye tunakula nae tunashinda nae sasa ni kitu gani kimewafanya wanaenda spidi hivyo lakini wale waliokuwa maadui zao wa siku nyingi leo wamekuwa marafiki zao,” alisema Makonda.

“Jambo la kwanza lililonishangaza nimevamia sio kweli wananchi wa mkoa wangu, sijawahi kuvamia kituo chochote kile cha runinga , nafasi yangu kama mkuu wa mkoa naweza kumuita mtu yoyote, nina maswali kama 50 kwenye lile neno ‘Kuvamia’ la kwanza wanasema nilivamia kipindi kirushwe wakati kipindi kile kilikuwa kiko live, Watanzania kama hapa tuko live hivi mtu unaweza kuvamia kweli wakati tuko live.”

Imeandikwa na Laila Sued na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents