Burudani

Sina beef na mtu, watoto wadogo ndio wenye beef – Msaga Sumu

Msanii wa Muziki wa Sengeli, Msaga Sumu amesema muziki huo unahitaji ushirikiano baina ya wasanii ili uweze kufika mbali na kubainisha ugomvi ndio una warudisha nyuma.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ‘Mwanaume Mashine’, ameiambia EA Radio ugomvi ni kitu ambacho asingependa kuona kinaendelea katika muziki huo.

“Mimi binafsi yangu huwa sina beef na mtu ila wenyewe kwa wenywe wanabeef, watoto wadogo walikuwa na beef lao na baada ya kujakupata nyimbo zao mbili tatu kuvuma wakaona washamaliza biashara,” amesema Msaga Sumu na kuongeza.

“Muziki huu wangeuua mapema lakini mwenyewe nashukuru Mungu kwa sababu mwanzoni nilikua stoi nyimbo kwa sababu ya longo longo za watoto, unaweza ukatoa wimbo wanakuja wanakuigizia sasa ile ubunifu ulikuwa hakuna,” amesisitiza.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents