Habari

Steps Entertainment yaja na tuzo ‘kimya kimya’ Bongo Movie Awards 2012 – 2013 zitakazotolewa June 15

Kampuni ya utayarishaji na usambazaji wa filamu nchini, Steps Entertainment imeandaa tuzo ziitwazo ‘Bongo Movie Awards 2012 – 2013’ zitakazotolewa June 15 kwenye ukumbi wa Blue Pearl Hotel – Ubungo.

947101_581549065201609_830508885_n

Tuzo hizo zimekuja kimya kimya kwakuwa hakuna mchakato wowote uliotangazwa kuhusu tuzo hizo hadi leo ambapo wametangaza tarehe ya kutolewa kwake.

Tumejaribu kuongea na uongozi wa Steps kuhusu tuzo hizo lakini wamedai watatoa taarifa baadaye.

Inaonekana tuzo hizo zitahusisha filamu zinazoandaliwa na kusambazwa na kampuni hiyo tu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents