Habari

Suala la maadili sio jukumu la Rais peke yake – Ndalichako

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Dk Joyce Ndalichako amewataka wazazi na jamii kwa ujumla kusimamia nidhamu kwa wanafunzi na kuchukua hatua kwa wanafunzi kwa utovu wa nidhamu shuleni na kwamba suala la maadili ni la kila mtu.

image-2

Akizungumza Jumanne hii jijini Dar es Salaam, katika Mdahalo wa kujenga maadili Haki za binadamu, uwajibikaji utawala bora,mapambano dhidi ya rushwa, waziri Ndalichako amesema kuwa maadili si jukumu la rais pekee.

“Suala la kukuza na kusimamia maadili sio jukumu la rais peke yake, au jukumu la taasisi peke yake ni jukumu la jamii nzima, hivyo tunatakiwa sote kushirikiana kwa pamoja katika ngazi zote,” alisema.

Aidha Ndalichako amesema kuwa jamii imeshuhudia kuwepo kwa viashiria vingi vinavyoonyesha kuporomoka kwa maadili huku akidai kuwa si jambo njema kwa mustakabali mzuri wa taifa.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents