Habari

Swahili Fashion Week kuanza Ijumaa hii, zaidi ya wabunifu 15 wa kimataifa kuonesha mavazi yao

Zaidi ya wabunifu 15 wa mavazi wa kimataifa, wataonesha mavazi yao katika onesho la sita la ‘Swahili Fashion Week’ linaloanza Ijumaa hii ya December 6 hadi December 8 kwenye ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Mavazi na Mitindo Bw. Honest Arroyal akifafanua Jambo kuhusiana na Wabunifu watakaoonesha Mavazi yao katika Swahili Fashion Week
Mratibu wa Mavazi na Mitindo Honest Arroyal akifafanua Jambo kuhusiana na Wabunifu watakaoonesha Mavazi yao katika Swahili Fashion Week

Wabunifu hao wanatoka kwenye nchini 9 wakiwa pamoja na wabunifu 27 wa Tanzania watakaonesha nguo mbalimbali zitakazovaliwa mwaka 2014 Afrika Mashariki.

Wabunifu watakaoonesha mavazi yao Ijumaa ni pamoja na Cynthia Schiming – Namibia, Yvonne Ndawana – Zimbabwe, Afrostreet Kollektion – Kenya na Michelle Ouma – Kenya. Siku ya pili (7th Dec 2013) watakaoonesha ni pamoja na Kutowa Designs –Zambia, Walove – Kenya, Lulu Philista Oniang’o – Kenya, Terrance Chipembere –Zimbabwe, Carla Silva – Angola, 2Heads by Atsu – Ghana, Estelle Mantel Clothing – Zambia, Chizika – Czech Republic, Taati Sibolile Maison – Namibia na Palse South Africa – South Africa.

Afisa Habari na Mahusiano wa Swahili Fashion Week Bi Esi Mgimba akielezea Kuhusu Shopping Festival katika maonesho ya Swahili Fashion Week
Afisa Habari na Mahusiano wa Swahili Fashion Week Bi Esi Mgimba akielezea Kuhusu Shopping Festival katika maonesho ya Swahili Fashion Week

Siku ya tatu (8th Dec 2013) watakaonesha mavazi ni Arapapa by Santa Anzo – Uganda, Hafeni Frans – Namibia, MO Creations & Couture – Zambia, Suhaa Schmitz – Rwanda na David Tlale – South Africa.

Kwa upande wa Tanzania wabunifu wa mavazi watakaonesha mkusanyiko wa nguo zao ni pamoja na H &A Dress to Impress, Tanzania Mitindo House, Anne Kiwia Dar es Salaam, Na Kadhalika, Can Wear and Handmade from Tanzania, Malleni Designs, House of Wellu, Keramiti, Catherine Mlowe, Jasmine Greca Sinare, Lucky Creations na Ailinda Sawe.

wabunifu wakiwa katika picha ya pamoja na afisa habari na mahusiano wa Swahili fashion Week Esi Mgimba na Events and sponsorship Manager wa Vodacom Ibrahim Kaude katika Mkutano na Wana habari
Wabunifu wakiwa katika picha ya pamoja na afisa habari na mahusiano wa Swahili fashion Week Esi Mgimba na Events and sponsorship Manager wa Vodacom Ibrahim Kaude katika Mkutano na Wana habari

Siku ya pili watakuwepo Martin Kadinda, Hameed Abdul, Khadija Mwanamboka, Dominick Godfrey, Yechi & Yuchi, PSJ Couture na Mgece Makory.

Siku ya tatu watakaokuwepo ni Eve Collections, An Nisa Abayas, Eskado Bird, Kiki’s Fashion, Asia Idarous Khamsin, Gabriel Mollel, Zaidi Africa, na Jamilla Vera Swai.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents