Habari

Swali la MSD kukosa baadhi ya dawa zinazohitaji kwa wagonjwa latinga bungeni

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa endapo madawa yatakosekana katika maghara ya MSD yaliyopo kwenye kanda na Makao Makuu ya MSD. MSD anapaswa kumtaarifu mteja ndani ya siku moja ya kazi ili akanunue kwa watu binafsi.

Akizungumza leo bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Hamis Kigwangalla wakati akijibu swali la Mbunge Mary Chatanda aliehoji Je? Serikali imetoa maelekezo gani pale ambapo MSD wamekuwa hawana baadhi ya dawa zinazohitaji kwa wagonjwa?.

Dkt Kigwangalla akiijibu swali hilo amesema “Sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013(140) ina vitaka vituo vyote vya kutolea huduma za afya MSD maoteo ya mwaka mwezi Januari ya kila mwaka ili kuiweze MSD kuyaingiza kwenye mpango wake wa manunuzi vituo vya kutolea huduma za afya vinatakiwa kununua mahitaji yake kutoa MSD.”

“Pale endapo madawa hayo yatakosekana katika maghara ya MSD yaliyopo kwenye kanda na Makao Makuu ya MSD, MSD anapaswa kumtaarifu mteja ndani ya siku moja ya kazi ili akanunue kwa watu binafsi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents