Fahamu

TAFITI: Viumbe hai vyote vitakufa ila kiumbe huyu ataishi mpaka mwisho wa dunia

Wengi wetu katika imani tunaamini kuwa ipo siku ya mwisho wa Dunia ambapo Mungu atakuja kuwahukumu wanaadamu, Lakini sio kwa Wanasayansi hao wanaamini kuwa mwisho wa Dunia ni ile siku ambayo viumbehai vyote vitakufa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kama kuongezeka kwa joto, kushuka kwa vimondo, matetemeko ya ardhi na majanga mengine na huo ndiyo utakuwa mwisho wa dunia.

Tardigrades (pictured) will be the last surviving species on Earth and could live through any doomsday event, scientists have claimed
Muonekano wa kiumbe aina ya (Tardigrade) ambao wataishi mpaka mwisho wa Dunia

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza wamegundua kiumbe hai kijulikanacho kwa jina la Tardigrade ambacho kinauwezo wa kuishi mpaka miaka bilioni 10 na kuhimili kila aina ya misukosuko ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Watafiti wamesema Viumbe hao wanauwezo wa kuishi bila kula kwa miaka 30 na wanauwezo wa kukaa kwenye joto la kiwango cha Celsius 150°C kwa miaka 20.

Viumbe hao wadogo wadogo kimaumbile wenye magamba magumu wanapatikana kwa nadra sana baharini na ndio viumbe hai pekee duniani wenye uwezo wa kuhimili miale ya kiwango cha 5000-6200 (Gamma Ray) ambacho huaribu seli na tishu za viumbe hai.

Dr Rafael Alves Batista ni moja ya waliohusika kwenye utafiti huo na ni mkuu wa Idara ya Fizikia katika chuo cha Oxford amesema lengo la utafiti huo ni kubaini kiumbe hai kitakachokuwa cha mwisho kuishi baada ya viumbe hai vyote kufariki.

Kila kiumbe hai kinakufa lakini imetupasa kufikiria zaidi sio tuu kwa binadamu bali hata viumbe wengine kwani ipo siku dunia hii itakuwa sio sehemu salama kwa viumbe hai na wote watakufa ila kwa viumbe hawa wa maajabu (Tardigrades) atabaki hai mpaka jua lidondoke“,amesema Dr Rafael Alves Batista kwenye mahojiano yake na Gazeti la Daily Mail.

Dr David Sloan ni msaidizi wa Idara ya Utafiti katika Chuo Kikuu cha Oxford amesema wamefikia hatua hiyo ya kufanya utafiti baada ya kugundua kuwa binadamu wanaamini kuwa hao ndiyo watakuwa viumbe wa mwisho kuishi duniani kumbe sivyo ndivyo.

Binadamu wanaamini hao ndiyo watakuwa viumbe wa mwisho kuishi kumbe sivyo ndivyo na kwa utafiti huu nadhani wamepata mwanga kuwa hao ni viumbe dhaifa sana kuhimili majanga makubwa ukilinganisha na baadhi ya viumbe“,amesema Dr David Sloan.

Watafiti hao wamesema utafiti huo uliofanyika kwa miaka 10 huenda ukawa ni wa kwanza tuu kwani viumbe wengi wanaoishi majini wanauwezo wa kukaa miaka mingi kuliko wale wa nchi kavu.

Tazama video ya kiumbe huyo hapa chini kama ilivyorekodiwa kwenye utafiti huo.

By Godfrey Mgallah

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents