Fahamu

Taifa la Rwanda lampokea mtu asiye na uraia wa taifa lolote

Rwanda imetangaza kukubali mtu asiye na uraia wa taifa lolote kwa sababu za kibinamu Adham Amin Hassoun ambaye alihamishwa kutoka Marekani baada ya kukamilishi hukumu yake jela.

Bwana Hassoun mwenye umri wa miaka 58 alihamishiwa Rwanda mapema wiki hii kulingana na makubaliano ya 1954 juu ya watu wasiokuwa na utaifa kama mtu ambaye hatambuliwi na taifa lolote kama raia wake. Taarifa ya serikali ya Rwanda inasema kuwa Hassoun alikubali kwa hiari kuhamia nchini Rwanda.

Ni kwanini hakutambuliwa na taifa lolote duniani?

Adham Hassoun ni Mpalestina aliyezaliwa katika taifa la Lebanon ambaye aliamua kuishi nchini Marekani katika miaka ya 1980.

Alifanya kazi kama mtaalamu wa programu za kompyuta. Baada ya mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Marekani ya Septemba 11 alipatikana na hatia chini ya sheria ya uzalendo kwa michango yake ya misaada kwa shirika la msaada la Kiislamu ambalo liliyaunga mkono makundi yaliyohusika katika ugaidi katika Chechnya na Bosnia.

Anaripotiwa pia kuhudhuria ibada katika msikiti mmoja na José Padilla, Mmarekani aliyekamatwa mwaka 2002 kwa kuhusika na njama za kulipua kile kilichoitwa ”bomu chafu” nchini Marekani.

Mchoro wa picha wa Adham Amin Hassoun (wa pili kutoka kushoto) akiwa mahakamani
Mchoro wa picha wa Adham Amin Hassoun (wa pili kutoka kushoto) akiwa mahakamani

Hassoun alipatikana na hatia ya kuunga mkono ugaidi, ingawa hakushutumiwa kuhusika binafsi katika viendo vya gasia.

Alikamilisha hukumu yake gerezani mwaka 2018, lakini kwasababu hana uraia , hakuweza kurejeshwa kokote.

Kulingana na sheria, Marekani iliendelea kumuweka mahabusu na haikutumia kipengele cha sheria ya uzalendo.

Hatahivyo majaji nchini Marekani walipinga madai ya serikali ya Marekani kwamba ni tisho kwa taifa, lakini hawakuwa na jibu la ni wapi anaweza kwenda iwapo angeachiliwa .

Rwanda ilikubali kumpokea nchini mwake kwa misingi ya kibinadamu, na kwa makubaliano na Hassoun na kutokana na hofu ya mataifa mengine na kumruhusu kuishi nchini humo.

Wahamiaji wamewasili Jumatatu asubuhi mjini Kigali Rwanda
Wahamiaji kutoka Libya Kigali kutoka Libya walipewa makazi

Hii si mara ya kwanza kwa serikali ya Rwanda kuwapokea watu wasio na utaifa kutoka maeneo mbali mbali ya dunia ambapo iliwahi kufanya hivyo miaka ya nyuma.

Mwaka jana Rwanda iliwapokea na kuwapatia uraia zaidi ya wahamiaji 300 waliokua wamezuiliwa nchini Libya baada ya kuyakimbia mataifa yao, kulingana na Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Chanzo BBC

https://www.youtube.com/watch?v=T8hYoJ7LxZs&t=130s

https://www.youtube.com/watch?v=xFPX-6P2jYQ

https://www.youtube.com/watch?v=gsZofW7NIaM

https://www.youtube.com/watch?v=nxzMGYQ-o74&t=9s

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents