Habari

Baada ya China kufunga Ubalozi wake Marekani nao wafunga ubalozi wao China

Huku zikiwa zimesalia saa kadhaa kabla ya kufikia Jumatatu asubuhi ambao ndio muda wa mwisho kwa wafanyakazi wa ubalozi huo wanaonekana wakibeba maboksi ya makablasha yao na mifuko ya takataka.

Wakati huo huo, umati wa wakazi wa eneo hilo umekusanyika nje ya ubalozi huo, ukiwa umebeba bendera za China na kupiga picha.

China ilichukua hatua ya kufunga ubalozi huo kujibu hatua ya Marekani kuufunga ubalozi wake mdogo wa Houston, Texas, wiki iliyopita.

Baada ya muda wa mwisho uliowekwa wa saa 72 kwa wanadiplomasia wa Uchina kuwa wameondoka Houston kumalizika Ijumaa, taarifa zinasema wanaume walionekana kuwa ni maafisa wa Marekani walifungua kwa nguvu mlango ili kuingia ndani ya ubalozi huo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alisema kuwa serikali ya Marekani mjini Washington iliamua kuchukua hatua hiyo kwasababu Beijing ilikua ”inaiba” akili miliki.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Uchina Wang Wenbin alijibu akisema hatua ya Marekani “mkanganyiko wa uongo wa chuki dhidi ya Uchina”.

Hali ya wasiwasi imekua ikiongezeka kati ya nchi hizo mbili zenye nguvu za nyuklia juu ya masuala mbalimbali :

  •  Utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump umekua na msuguano mara kadhaa na Beijing juu ya janga la virusi vya corona
  • Washington pia ililaani hatua ya China ya kuweka sheria mpya tata ya usalama katika Hong Kong.
  • Wiki iliyopita, mwanaume wa Singapore alikiri katika mahakama ya Marekani kufanya kazi kama jasusi wa China.
  • Pia wiki iliyopita, Wachina wanne walishitakiwa katika kesi tofauti na idara ya vibali vya usafiri (visa) ya Marekani kwa wizi wa visa kwa madai kwamba walidanganya kuhusu kuhudumu katika jeshi la China.

Ni taarifa zipi za hivi punde kutoka Chengdu?

Vyombo vya habari vya taifa la China vimekua vikionesha picha za malori yakiondoka katika ubalozi mdogo wa Marekani, na wafanyakazi wa ubalozi huo wakiondoa vitu kutoka kwenye jengo la ubalozi.

Makumi kadhaa ya polisi wa China wamekuwa wakipelekwa nje ya ubalozi huo, wakiwataka watu waliokusanyika nje kushuhudia kinachoendelea kuondoka na kujaribu kuzuia vitendo vya uchokozi .

Kundi la watu nje ya ubalozi mdogo wa Marekani

Hatahivyo, sauti zilizikika za watu waliokua wakizomea wakati basi likiondoka nje ya jengo hilo siku ya Jumapili, zimeeleza taarifa za shirika la habari la AFP.

Wakati wanadiplomasia wa China walipoondoka kwenye ubalozi wao Bouston kwa mara ya mwisho walizomewa na waandamanaji.

Ramani

Ubalozi mdogo wa Chengdu – ulianzishwa mwaka 1985 -na uliwakilisha maslahi ya Marekani katika eneo kubwa la Kusini-Magharibi mwa China, likiwemo jimbo linalo jitawala la Tibet, ambako kumekua na shinikizo la muda mrefu la kutaka uhuru wake.

Wengi wa wanadiploamasia zaidi ya 200 ni wafanyakazi walioajiriwa ambao ni raia wa China.

Huku likiwa na ukuaji wa viwanda na sekta ya huduma , jimbo la Chengdu linaangaliwa na Marekani kama eneo linalotoa fursa kwa mauzo ya nje ya bidhaa za kilimo, magari na mashine.

Baada ya kufungwa kwa ubalozi huo, Marekani itakuwa na balozi ndogo nne ndani ya China na ubalozi mkuu katika mji mkuu Beijing. Pia ina ubalozi mdogo Hong Kong, ambalo ni koloni la zamani la Uingereza.

China ilipoteza ubalozi wake mdogo wa Houston wiki iliyopita, lakini bado ina balozi ndogo nne nchini Marekani na ubalozi wake mkuu uliopo katika mji mkuu wa Marekani Washington DC.

Polisi wakilinda eneo la ubalozi

Ni kwanini kuna hali ya wasi wasi kati ya China na Marekani?

Kuna mambo kadhaa yanayohusika. Maafisa wa Marekani wanameishutumu China kwa kusambaza Covid -19 duniani. Zaidi ya hayo binafsi rais Trump amedai, bila ushahidi, kwamba virusi vilianzia katika maabara ya China katika mji wa Wuhan.

Na, katika kauli ambayo haina ushahidi, msemaji wa wizara ya ambao ya nje wa Uchina alisema mwezi Machi kwamba jeshi la Marekani huenda lilileta virusi Wuhan.

Marekani na China pia zimekua na vita vya ushuru tangu mwaka 2018.

Kwa muda mrefu Bwana Trump amekua akiishutumu China kwa kuwa na utendaji usio wa haki wa kibiashara na wizi wa hakimiliki, lakini mjini Beijing kuna mtizamo kuwa Marekani inajaribu kukabiliana na kupanda kwake kama taifa lenye nguvu za kiuchumi dunaini.

Marekani pia imeweka vikwazo dhidi ya wanasiasa wa Kichina ambao inasema wanawajibika na ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya Waislamu walio wachache katika eneo la Xinjiang.

China inashutumiwa kwa kuwaweka mahabusu watu wengi, mauaji ya kidini na kufunga uzazi kwa lazima waislamu wa jamii ya Uighur na wengine. Serikali ya Beijing imekanusha madai hayo na inaishutumu Marekani kwa ”kuingilia vibaya”masuala yake ya ndani ya nchi.

Chanzo China.

https://www.youtube.com/watch?v=xFPX-6P2jYQ

https://www.youtube.com/watch?v=gsZofW7NIaM

https://www.youtube.com/watch?v=nxzMGYQ-o74&t=9s

https://www.youtube.com/watch?v=QPgHWYKwam8&t=3s

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents