Burudani

RECAP: Wasanii wa Nigeria, Afrika Kusini hawapendi Bongo Fleva, Wanaiogopa na kuipinga (Video)

RECAP: Wasanii wa Nigeria, Afrika Kusini hawapendi Bongo Fleva, Wanaiogopa na kuipinga (Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameizungumzia kauli ya Rapa wa Afrika Kusini Cassper kuwa hajui nyimbo za Tanzania.

@el_mando_tz anasema Cassper amekataa kuupa promo muziki wa Tanzania lakini kimoyo moyo anaufatilia sana.

Amevyotua Aiport alisema anawafahamu Harmonize, Diamond, Marioo na DJ Vasley tena anamjua Marioo kwa sababu kuna wimbo wake umefanya vizuri sana kwao.

Siku ya pili anasema hajui wimbo wowote, kauli hiyo inaonyesha ishara tosha kuna chuki na muziki wa Bongo Fleva.

Ukweli ni kwamba mataifa kama Nigeria, Afrika Kusini wanapiga vita muziki wa Bongo Fleva na wasanii wake na ndio maana hata mitandaoni Wanigeria wanasema hawawajui wasanii wa Tanzania.

Kuna Trend ipo TIKTOK watu wanataja wasanii 10 bora Afrika ila Wanigeria wakiona msanii wa Tanzania wanasema hawawajui kabisa.

Wanaihofia sana Tanzania kimuziki, Watanzania wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuusapoti muziki wao.

Cassper hawezi kututoa kwenye reli.

Unakubaliana na @el_mando_yz kwa asilimia ngapi??

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

 

 

Host: @el_mando_tz Cameraman @samirkakaa

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents