Habari

Taifa Queens yaendeleza ubabe nchini Singapore, yashinda mechi 3 mfululizo na kuongoza katika kundi lake

TIMU ya Taifa ya Netiboli ‘Taifa Queens’ imeendeleza wimbi la ushindi kwenye michezo ya kimataifa ya netiboli inayoendelea nchini Singapore.

Jana Taifa Queens imewatandika wenyeji Singapore magoli 51 kwa 24.

Katika mechi mbili za kwanza, Taifa Queens iliichapa Sri Lanka mabao 67 kwa 51 na kuitandika Malaysia mabao 61 kwa 34.

Kutokana na matokea hayo, Tanzania sasa inaongoza kwenye kundi lake ambalo linajumuisha nchi za Namibia, Malaysia na Sri Lanka.

Kikosi hicho kinachoundwa na wachezaji kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kilipata maandalizi ya kutosha baada ya kukaa kambini mjini Morogoro kujiandaa na michuano hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents