Burudani

Tamasha La Swahili Hip Hop Summit Laanza kwa Kishindo

Tamasha maalum kwa ajili ya wana Hip Hop na Rap kwa kutumia ghani na lafudhi ya Kiswahili also known as “Swahili Hip Hop Summit” jana ilizinduliwa rasmi katika kituo cha utamaduni cha watu wa Ufaransa, Alliance Francaise na kukonga nyonyo za watu waliojitokeza.

Tamasha hilo ambalo limeandaliwa maalum kama sehemu ya maonyesho ya kazi za wasanii wa Hip hop ambao mara nyingi wamekuwa wakilalamika kubaguliwa na kutengwa lilipata ugeni wa waheshimiwa mabalozi wa Ufaransa na Uswisi majira ya saa 4 asubuhi, ambapo walitembelea na kukagua kazi mbali mbali za kisanii zinazoonyeshwa katika ukumbi wa mikutano na matukio katika kituo hicho cha utamaduni.

Tamasha hilo limegawanyika katika sehemu kuu mbili, ambazo ni maonyesho (exhibition) na burudani(entertainment), huku likifuata misingi mikuu ya nguzo tano za Hip hop ambazo ni pamoja na kughani mitindo huru (Free Style), Kucheza Dance kwa Mitindo huru (Break Dance), Sanaa ya uchoraji kwa kutumia makopo ya rangi ( Grafitti), Kuonyesha uwezo wa ku Dj ( Dj-ing), na ujuzi ama uelewa wa elimu ama misingi ya Hip-Hop.

Kwa asilimia kubwa maonyesho hayo yanaonekana kukubalika zaidi na wasanii wa hip hop toka Arusha ambao kwa jana walikuwepo wengi zaidi.

Bidhaa mbali mbali toka makundi tofauti ya wasanii toka Arusha wakiongozwa na JCB zilikuwepo katika maonyesho.

Aidha katika tamasha hilo, vipengele vya mitindo huru (free Style) ilitawaliwa na vijana wawili ambao ni leloo na Mtaganda, wakati Dj-ing, na Break dance ikitawaliwa na wakongwe wawili wa zamani katika fani hizo Bwana Diga Diga ambaye anajulikana zaidi Double D na katika fani ya Break Dance na John Dilinga ambao waling’ara na kuamsha shangwe za mara kwa mara kwa uwezo mkubwa walionyesha katika fani zao.

Tamasha hilo linaingia siku ya pili leo, ambapo kutakuwa na maonyesho na burudani zaidi mida ya jioni huku ikitarajiwa kuhutubiwa na balozi wa Ufaransa nchini Bwana Marcel Escure.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents