Shinda na SIM Account

TANESCO yatoa siku 4 kwa wadaiwa sugu

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limetoa siku 4 kwa wateja wao wote wale wadaiwa sugu kuanzia tarehe 12 Januari mwaka huu hadi Januari 15, mwaka huu wawe wamelipa madeni yao.

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO) TAARIFA KWA UMMA – WADAIWA SUGU

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tunautaarifu Umma na Wateja wetu wote kuwa, tumetoa muda wa siku nne (4) kuanzia Januari 12, 2018 hadi siku ya Jumatatu Januari 15, 2018 kwa wadaiwa sugu wawe wamelipa madeni yao.

Baada ya muda huo kuisha Shirika litasitisha Huduma ya umeme dhidi ya Wateja watakaoshindwa kulipa madeni ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zingine za kisheria.

Ofisi za TANESCO zitakuwa wazi siku ya Jumamosi Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 9:00 Mchana.

Mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/

IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO

TANESCO MAKAO MAKUU

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW